• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

MADAKTARI BINGWA NA WAHUDUMU WA AFYA ZAIDI YA 450 KUTOA MATIBABU BURE MKOANI ARUSHA...

Posted on: June 22nd, 2024

Na Elinipa Lupembe


Madaktari bingwa na watoa huduma za afya zaidi ya 450 kutoka kwenye Hospitali na Taasisi takribani 40 za afya nchini Tanzania wanatarajiwa kutoa huduma za vipimo na matibabu bure kwa wakazi wa Mkoa wa Arusha kwa siku saba mfululizo kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo Juni 24, 2024.

Kauli hiyo imetolewa mapema leo Jumamosi Juni 22, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda mara baada ya kukagua maandalizi ya Kliniki hiyo ya afya inayotarajiwa kuzinduliwa Jumatatu ya wiki ijayo kwenye viwanja vya michezo vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Mkuu wa Mkoa ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wote wa Arusha kujitokeza kwa wingi kwenye Kliniki hiyo, akitoa hakikisho la vipimo, matibabu na dawa bure kwa kila mwananchi atakaebainika na kugundulika kuwa na magonjwa na maradhi ya aina mbalimbali.

"Ndugu zangu asiwaambie mtu, kwenye suala la afya kuna watu wameuza nyumba zao, kuna watu wameuza viwanja, kuna watu wamefilisika biashara zao katika kupambana kuuguza ndugu zao na kuna nyakati nyingine kuna ndugu zetu wameshindwa hata kukomboa miili ya ndugu zao kutokana na madeni ya gharama za matibabu. Neema hii ambayo Mungu ametupa tukaitumie na mikono ya watumishi wa Mungu ikafungue baraka ili tukapate afya kupitia madaktari wetu hawa bingwa." Amesema Mh. Makonda

Kulingana na Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda, Hospitali na Taasisi zitakazoshiriki kwenye kliniki hiyo na kutoa madaktari wake bingwa ni pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya afya ya akili Milembe, Hospitali ya kanda KCMC, Hospitali ya Kanda Benjamin Mkapa, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Taasisi ya mifupa Moi pamoja na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Mawenzi, SAIFEE pamoja na hospitali na taasisi nyingine za ndani na nje ya Mkoa wa Arusha. @baba_keagan


Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.