Mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia ikiwa ni pamoja na madarasa yanayoongea yaliyosheheni michoro ya zana zenye rangi mbalimbali, na vifaa vya kuchezea, kwa pamoja vinaongeza ari na uwezo wa mtoto kujifunza pamoja na kumuwezesha mtoto kujifunza kwa wepesi na kwa haraka zaidi.
Serikali ya awamu ya sita, kupitia mradi wa BOOST, imezingatia vigezo vya mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia, kwa kujenga madarasa ya awali ya mfano kwenye shule za msingi nchini.
Mkoa wa Arusha, ni miongoni mwa mikoa nchini, ambayo imepata fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa ya awali ya mfano, madarasa ambayo licha ya kuonheza idadi ya wanafunzi kuandikishwa kuanza shule, imeongeza furaha kwa watoto pamoja na kuwafanya kupenda shule na kupunguza utoro shuleni.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.