Madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Karatu wameomba wadau wa maendeleo kushirikiana kwa pamoja kwaajili ya kufungwa mifumo ya kieletroniki ya ukusanyaji mapato (GoTHOMIS) katika vituo vya afya vituo 41 vilivyopo wilayani hap.
Ombi hilo, limetolewa na madiwani hao katika Baraza Maalum la kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2022/23, ambapo Diwani wa Kata ya Baray, Elitumaini Magnus amesisitiza ufungwaji wa mfumo huo ili kuongeza kasi ya ukusanywaji mapato hayo kwani hivi sasa halmshauri hiyo imefunga mfumo huo katika vituo vya afya 7 kati ya vituo 34 ambayo bado havijafungwa.
Naye Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Karatu, Dkt. Victor Kamazima amekiri ni kweli vituo vituo 7 tu kati ya 34 ndio vimefungwa mfumo huo wa GoTHOMIS na kuongeza kuwa mwaka huu wa fedha kabla haujaisha wametenga kiasi cha fedha shilingi milioni 34 kwaajili ya kununua vifaa vya awali ikiwemo kompyuta kwaajili ya kuanzia.
Dkt. Kamazima ameongeza kuwa, kwa mwaka ujao wa fedha wametenga kiasi cha fedha shilingi milioni 43 kwaajili ya ufungaji wa vifaa vya kisasa kati ya vituo 41 vilivyobaki na kusisitiza kuwa mchakato wa kufunga mfumo huo unaendelea kadri bajeti itakavyowaruhusu kulingana na mapato wanayokusanya katika kila kituo cha afya.
Hata hivyo, Madiwani hao wamependekeza miradi iliyokaa kwa muda mrefu bila kutekelezwa itekelezwe kwa kubadilishiwa matumizi au fedha zitafutwe ili kuhakikisha miradi hiyo itekelezwe ikiwemo bweni la shule ya sekondari ya Ganako na kituo cha afya cha Mbuganyekundu kikamilike.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Musa amesisitiza hadi Septemba mwaka huu mfumo huo ufungwe kwani unapoteza mapato mengi kwa serikali na kusisitiza madeni ya watumishi na wazabuni kulipwa kwa wakati ili kuondoa malalamiko kwa watoa huduma katika wilaya hiyo.
"Lipeni madeni ya wazabuni na watumishi ikiwemo utunzaji wa kumbukumbu za wadaiwa wenu maana kuna mahali ukifuatilia kumbukumbu za madeni wanayodai wazabuni mengine huyaoni hivyo hakikisheni mnalipa mnayodaiwa". Amesema.
Kwa upande wake, Mwekahazina wa Halamshauri ya wilaya hiyo, CPA. Liberatus Kazungu, amesema halmshauri ya hiyo
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.