Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw.Misaile Musa akiongea na kuwakaribisha Maafisa Elimu Sekondari na Msingi pamoja na baadhi ya Wakuu wa Shule waliongozwa na Afisa Elimu Mkoa wa Kagera ambao wapo Mkoani Arusha kwa ziara ya kimafunzo ya kujifunza mafanikio ya Kielimu ambayo Mkoa wa Arusha umeyafikia kwa kuwa kati ya Mikoa bora inayofanya vizuri katika ufaulu wa Mitihani ya Shule za Sekondari na Msingi kwa miaka mingi mfululizo.
Maafisa Elimu hao watapata fursa ya kujionea mitambo ya uchapaji Mitihani ya majaribio kwa Shule za Sekondari na Msingi inayitumika kuwapima Mwanafunzi kabla ya Mitihani ya Kitaifa kufanyika.
Aidha watatembelea Shule ya Msingi Kisimani na Meru zilizopo Jiji la Arusha na Shule ya Msingi Enaboishu na Shule ya Sekondari Mwandet iliyopo Arusha DC Wilayani Arumeru.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.