• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

MAFANIKIO YA AWAMU YA SITA YANATOKANA NA MARIDHIANO, AMANI, UTULIVU NA USHIRIKIANO BAINA YA WATANZANIA..

Posted on: December 14th, 2023

Na Elinipa Lupembe.


Imeelezwa kuwa, mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hasaan, yanatokana na maridhiano baina ya watanzania yanayoleta amani, utulivu na mshikamano na kuipa nafasi Serikali, kujikita kwenye kuleta maendeleo huku wananchi wakielekeza mawazo yao katika kufanya kazi za uzalishaji na kulijenga taifa.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, wakati akifungua  kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), na kusema kuwa, Serikali ya awamu ya sita, imefanya juhudi kubwa za kurejesha hali uzalendo unaobeba utaifa kwa watanzania wote, na kusababisha amani na utulivu nchini, mambo ambayo yalianza kupotea.


"Miradi mikubwa mnayoiona inayotekelezwa nchini, hususani kwenye mkoa wetu wa Arusha, katika sekta zote, tunashuhudia shule zinajengwa, barabara, miradi ya maji, na maendeleo ya kila aina, Utalii kupitia Serikali na sekta binafsi, yote ni matunda ya ushirikiano baina ya wananchi, viongozi na Serikali kwa pamoja wakiwa wanania mamoja" Amesema Mhe. Mongella


Amewaomba wananchi wa mkoa huo, kuendelea kudumisha ushirikiano miongoni mwao, kwa kuweka mbele utaifa na kujikita zaidi katika kufanya kazi ili kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa na kuwasihi viongozi wote wa jamii, dini, mila na Serikali kushirikiana  katika shughuli zote za maendeleo na ujenzi wa Taifa.


Naye Katibu wa Chama cha ADP mkoa wa Arusha, Mussa Bayo, amempongeza mkuu wa mkoa wa Arusha, kwa kudumisha umoja na msikamano wa wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa kwa kuwa wanajenga nyumba moja.


"Nikupongeze mkuu wa mkoa, wewe ni kiongozi bora, umekuwa ukitualika kwenye vikao vya ushauri na sisi tunatoa ushauri kwa maendelo ya taifa letu na huu ndio mshikamano anaoutaka mama Samia, Wakuu wa wilaya igeni mfano " Ameweka wazi Katibu huyo wa ADP


Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM , Mkoa wa Arusha, Loy Ole Sabaya, licha ya kupongeza viongozi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo amewasihi kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili thamani ya fedha zilizotolewa na serikali iweze kuonekana.


"Mradi ukikaa muda mrefu hata thamani ya fedha inashuka, bei ya vitu itabadilika na kusababisha ucheleweshwaji ambao unaondoa kabisa maana na malengo ya mradi husika, hivyo niwasihi wakurugenzi na wakuu wa Idara kusimamia miradi yote na ikamilike kwa wakati". Amesema Ole Sabaya.


Awali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Mussa, amewasilisha hali ya uharibifu wa mazingira na miundombinu ya barabara unaotokana na ujenzi kwenye vyanzo vya maji na kingo za mito pamoja na uchimbaji wa moram kwenye vilima katika  halmashauri za Arusha, Meru na Jiji la Arusha.


#ArushaFursaLukuki



Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.