Magari zaidi ya 300 chapa ya Land Rover yameanza safari ya pamoja kuelekea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Arusha ikiwa ni siku ya pili ya Tamasha la Land Rover Jijini Arusha na matarajio ni kuiweka rekodi nyingine ya dunia ya kuwa na Magari zaidi ya 300 yanayoingia kwenye hifadhi ya wanyamapori kwa wakati mmoja.
Jana wakati wa siku ya kwanza ya Land Rover Festival, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda aliuthibitishia Umma kuwa Arusha na Tanzania imefanikiwa kuweka rekodi ya kuwa na msafara mrefu zaidi wa magari chapa moja ya Land Rover, magari yaliyofikia idadi jumla ya 1034 na hivyo kuivunja rekodi iliyoshikiliwa na Ujerumani kwa kuwa na magari 632 miaka sita iliyopita.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.