Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela ameitaka mahakama ya Afrika ya haki za binadamu ikafanye kazi zake kwa haki ili kuweza kupambana na matatizo yaliyopo katika bara la Afrika.
Aliyasema hayo alipokuwa akimwakilisha, Rais Samia Suluhu, katika hafla ya kuchagua na kuwaapisha majaji wapya wa Mahakama hiyo.
Aliahidi ushirikiano ili kufanikisha malengo ya nchi wanachama na mahakama katika kuimarisha haki za binadamu.
Amesema amani na utulivu wa nchi yoyote popote Duniani inategemea sana mahakama kuwa za haki, kwani wanapambania matatizo ya Afrika ili bara liwe na amani na kujiletea maendeleo kwajili ya ustawi wa nchi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.