Makamu wa kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewasili mkoani Arusha kwa Ndege ya shirika la Unity Air Zanzibar 5H-KIH na kupokelewa na Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi na Kamati ya Ulinzi Mkoa, kwenye uwanja wa Ndege Arusha, jioni ya leo Agosti 31, 2024
Mhe. Othman Masoud yuko mkoani Arusha, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Mbio za "Mbio za SAME QUALITY FOUNDATIONCLEFT MARATHON MSIMU WA SITA" zitakazofanyika kesho tarehe 01 Septemba, 2024 mkoani Arusha, mbio zenye lengo la kuchangia upasuaji wa watoto wenye mdomo sungura nchini.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.