Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameahidi kusimamia kikamilifu maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wakazi wa Ngorongoro ikiwemo kuhakikisha kuwa wananchi hao wanapata huduma zote za kijamii.
Leo August 23, 2024, Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo mara baada ya kutolewa kwa maelekezo ya Mhe. Rais yaliyowasilishwa na Waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu, Sera,Bunge na utaribu Mhe. William Lukuvi, wakati walipokuwa wakizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro inayopatikana mkoani Arusha.
"Hautahamishwa kwenye Kijiji, hautahamishwa kwenye nyumba yako na zile huduma muhimu ambazo zilikuwa zimezuiwa, Maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa nchi na Mwenyekiti wa CCM ametaka huduma hizo zirudishwe haraka iwezekanavyo", amesema Mhe. Makonda.
Mhe. Paul Christian Makonda ametumia fursa hiyo pia kuwataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi kwenye mchakato wa kujiandikisha kwenye daftari la mpigakura pamoja na kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.