Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Meru kuhakikisha ujenzi wa majengo katika vituo mbalimbali vya afya unakamilika na kuanza kazi mapema.
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akikagua ujenzi wa majengo hayo alipofanya ziara ya siku moja katika halmashauri hiyo.
Wananchi wanasubiri kupata huduma za afya katika vituo hivyo si vyema kama ujenzi utachukua muda mrefu na kusababisha usumbufu kwa wananchi.
"Hakikisheni vituo hivi vinakamilika kwa wakati na kuanza kazi ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma kwa karibu".
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Mwal. Zainabu Makwinya amesema ukaguzi wa ujenzi katika halmashauri hiyo huwa unafanyika mara 3 kwa wiki hivyo imepelekea kasi ya ujenzi kuongezeka.
Aidha, amesema kwa ziara ya Dkt. Kihamia imewapa nguvu zaidi yakusimamia ujenzi wa vituo hivyo vya afya na ameaidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa ili kuleta huduma bora kwa wananchi.
Nao, wajumbe wa kamati ya ujenzi ya kituo cha Afya Mareu Bi. Magdalena Israeli na Bi. Janeth Simoni wamemshukuru Rais Mama Samia kwa kutoa fedha za ujenzi wa kituo hicho cha Afya kwani kitapunguza hadha waliyokuwa wanaipata wanawake katika kupata huduma za afya.
Dkt. Kihamia amefanya ziara ya siku moja katika halmashauri ya Meru na kukagua vitua vya afya vitatu na hospitali ya Wilaya ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa majengo yanayojengwa katika maeneo hayo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.