*Afunga safiri kutoka Mbeya, kufuata huduma Kambi ya Madaktari Bingwa na Wabobezi Arusha*
_Aanza kupata Matibabu, kusafirishwa kwenda Muhimbili kwa gharama za serikali._
Mama mzazi wa mtoto Godson, anayesumbuliwa na kuoza viungo vya mwili wake, amelazimika kusafiri
zaidi ya 1000 kutoka Mbeya mpaka mkoani Arusha kwa lengo la kutafuta huduma ya matibabu ya kibingwa, hatimaye kutua kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta na kukutana na Kambi ya matibabu inayoratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda.
Familia ya Isaac Mwasakapwela wanauguza mtoto Godson kwa miaka saba sasa, akisumbuliwa na matatizo ya kuoza viungo vya mwili pamoja na kuchomoka kwa vipande vya nyama na mifupa, kiasi cha kutoa harufu mbaya inayosababisha kufukuzwa kwenye nyumba wanazopanga.
"Mume wangu ambaye ni baba wa mtoto huyu, alinikimbia baada ya kuona mtoto wetu ananyofoka ulimi, anadondosha masikio, miguu inaoza na kudondoka, mifupa inachomoka nikawa naiokota tu na akioza namkata kwa kiwembe na kutupa sehemu zinazooza. Akanikimbia yule mwanaume" amesema mama wa mtoto huyo Bi. Joyce Mwaipopo
"Kusema ukweli sijawahi kupokelewa vizuri kama hivi leo tangu mwanangu alipoanza kuumwa miaka saba iliyopita. Sijawahi! Naona wenzangu wamebahatika sana kwa Mungu kuwapa huyu baba (Paul Makonda) ili kuwasaidia. Mkuu wa wilaya yangu ananifahamu, Mkuu wa mkoa wangu ananifahamu lakini sikuwahi kufanikiwa kama hivi." Ameongeza Bi Joyce.
Katika hatua nyingine pia Familia hiyo inayoendeshwa na Bwana Isaac ambaye ni Dereva wa Bodaboda, wameshukuru kwa vipimo walivyovipata kwenye Kambi ya Matibabu inayoendelea kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid wakisema wamekuwa wakihangaika kutafuta fedha za kufanya vipimo hivyo kwa miaka saba bila ya mafanikio yoyote.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.