Na Elinipa Lupembe
Mama mwenye watoto 11 mkazi wa kata ya Mateves halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, kumsaidia mzigo mkubwa wa malezi ya watoto hao, kutokana na kuwa baba wa watoto hao, kufariki dunia na kumuacha akiwa mjane huku akihangaika na malezo ya watoto hao.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 39, ameomba kusidiwa ili aweze kumudu na kukabiliana na hali ngumu ya maisha inayomkabili katika kulea watoto hao, ambapo kati ya watoto hao yupo mtoto mwenye ulemavu pia ambaye ameomba kupatiwa Bima ya afya na kiti mwendo, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la soko la Kisongo Juni 04, 2024.
Mkutano huo umefanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, aliposimama kuwasalimia wananchi wa kata hiyo, wakati wa ziara yake mkoani Arusha Juni 02, 2024 na kumtaka Mhe. Makonda kurudi kwenye kata hiyo rasmi, ili kusikiliza na kushughulikia kero za wananchi hao wa kata ya Mateves.
#ArushaNaUtalii
#kaziinaendelea ✍
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.