Na Elinipa Lupembe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa zawadi ya sikukuu za mwaka mpya, maalum kwa ajili ya watoto wanaolelewa kwenye Makao mkoani Arusha.
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mhe. Rais, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mongella amesema kuwa zawadi hiyo ya vyakula, imetolewa na Mhe. Rais Samia, maalum kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya mwaka mpya 2024 kwa watoto hao.
Mhe.Rais ametoa zawadi hizo ikiwa ni ishara ya upendo, amani pamoja na moyo wake wa kipekee wa kuwajali watoto wenye mahitaji na waishio kwenye Makao ya kulelea watoto, ili na wao wajisikie kama walivyo watoto wengine wa kitanzania.
"Mhe. Rais amenituma kuleta zawadi hizi kwa niaba yake, kwa kuwa ni kawaida yake, ikifika msimu wa sikukuu hupenda kutoa, zawadi kwa watoto wanaolelewa kwenye Makazi yanayolea watoto wenye uhitaji nchini". ameweka wazi Mhe. Mongella
Aidha amewapongeza walezi wa watoto hao, kwa kazi kubwa wanyoifanya, kazi ambayo ina thamani na thawabu kubwa kwa binadamu na zaidi kwa Mwenyenzi Mungu, kazi ambayo wanaifanya kwa niaba ya Serikali.
Zawadi hii licha ya kuwa ni ishara ya upendo, pia inaonyesha namna Serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na walezi, kazi ambayo ni kuisaidia Serikali katika malezi ya watoto, hususani watoto hawa wenye mahitaji maalumu kutokana na changamoto nyingi zilizowafikisha hapo.
Akizungumza wakati wa kupokea zawasi hizo, Kiongozi wa Makao hayo, Mtawa. Marieta Muyegi, amemshukuru mama Samia na Serikali yake kupitia mkuu wa mkoa wa Arusha, kwa majitoleo ambayo yanaonesha upendo wa hali ya juu kwa watoto waishio kwenye makao.
"Tufikishie salamu zetu kwa Mama Samia, tunatambua mchango wa serikali kwa kuweka mazingira wezeshi ya kuwalea watoto wenye uhitaji nchini, vituo hivi vinafanya kazi kutokana na sera nzuri za Serikali ya awamu ya sita" Ameweka wazi Sista Marietha.
Hata hivyo watoto hao, wameshukuru kwa zawadi hizo, na zenye thamani kubwa kwao na kumuombea kwa Mwenyenzi Mungu amjalie kila lenye kheri katika maisha yake pamoja na uongozi wake.
Naye mtoto, Florentina Philip Mbisha, amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa zawadi hiyo na kumuombea kwa Mwenyenzi Mungu amzidishie pale alipotoa na kumzidishia Baraka nyingi katika maisha yake.
Awali, Mhe. Rais ametoa zawadi za chakula na kitoweo yenye thamani ya shilingi milioni 4.3 , kwenye vituo viwili vya makao ya watoto, Makao ya St. Gabriel ya jijini Arusha, Makao ambayo wanawalea watoto ambao wazazi wao wanatumikia vifungo katika magereza mbalimbali nchini na Makao ya Dhi Nureyn yaliyopo eneo la Ngaramtoni wilaya ya Arumeru.
Zawadi hizo ni pamoja na mchele, sukari, unga wa ngano na sembe, maharage, mafuta ya kula, juisi, boksi za biskuti na mbuzi wawili kwa kila kituo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.