Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Muhandisi Richard Ruyango amezindua maonesho ya nanenane Kanda ya Kaskazini katika Viwanja vya Themi Njiro kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Aruha Mhe.John Mongella.
Katika uzinduzi huo Mhe. Ruyango amewataka wakulima kutumia maonesho hayo kupata elimu sahihi juu ya Kilimo bora na ufugaji wa kisasa ili kuleta tija zaidi katika uchumi wao na nchi kwa ujumla.
Amesema, maonesho hayo yasichukuliwe kama mazoea tu bali yawe yenye kuleta tija kwao hasa katika kubadilisha ufugaji na Kilimo cha kizamani.
Maonesho ya nanenane Kanda ya Kaskazini yameanza Agosti 1 na yanatarajiwa kufungwa Agosti 8 yakiwa yamejumuisha Mikoa 3 ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.