Maelfu ya waombolezaji waliohudhuri kwenye misaa takatifu ya kuaga pamoja na mazishi ya aliyekuwa Katibu Tawala wa mkoawa Arusha, marehemu Richard Kwitega, wameelezwa maisha aliyoishi marehemu Kwitega ni ya ushuhuda kwa wengine, kifo chake kiwe funzo katika maisha ya kila mtu.
Akizungumza wakati wa kutoa salamu zake za pole, Naibu Waziri OR -TAMISEMI, mheshimiwa David Silinde, amesema kuwa maisha aliyoyaishi marehemu Kwitega ni maisha ya ushuhuda wa matendo yamayopaswa kufanywa na mtumishi wa Umma katika kutumikia wananchi pindi anapoaminiwa na serikali ma kupata madaraka ya kuwaongoza wengene pamoja na kuwatumikia wananachi.
"Kagika kipindi cha uhai wake na utumishi wake, mraehemu Richard aliwekeza katika utu, uzalendo na uadilifu, jambo linalotakiwa kufanywa na mtumishi wa Umama aliyepewa madaraka ya kuongoza na kuwatumikia wananchi, hivyo viongozi tuliopewa dhamana ya kuwatumikia wengine, niwajibu wetu kutenda kwa tunaowatumikia" amesisistiza Naibu Waziri Silinde.
Naye Mhashamu Askofu wa Jimbo la Geita, mhasham Askofu Flavian Kasala, amemuelezea marehemu Kwitega kuwa, aliishi maisha ya kujitoa kwa ajili ya wengine, na kuthibitisha kuwa ana heri anayetenda matendo ya imani ya kujitoa kwa ajili ya wengine na huu ni ushuhuda wa maisha ya marehemu Kwitega kwa kanisa, jamii na serikali aliyokuwa anaitumikia.
Mkuu wa mkao wa Arusha Mheshimiwa Idd Kimanta, amesema Serikali imepoteza mtu muhimu, hususani katika mkoa wa Arusha, mtu aliyependa kuwatumikia wananchi, aliyekuwa kiongozi alitekeleza majukumu yake kwa weledi mkubwa akijikita katika ubobevu wake katika masuala ya utawala.
Katibu Tawala wilaya ya Monduli, Robart Siankeni, amesema kuwa tutamuenzi marehemu Kwitega, namna ya kusimamia utawala bora na wajibikaji katika kuwatumikia wananchi, umuhimu wa kutekeleza mipango ya serikali kwa kusimamia miradi ya maendeleo, kubuni vyanzo vya mapato, kuchochea sekta ya utalii mkoani Arusha na pamoja na kusimamia amani na utulivu.
Naye mwakilishi wa famili, na Kagibu wa Rais, Ngusa Samike, amesema kuwa familia inamshuku Mungu kwa zawadi ya maisha ya marehemu Kwitega, alikuwa ni kiongozi wa familia, jamii na kuwa maisha yake yote aliishi kwa kuwatumikia watu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.