Mwenge wa uhuru utawasili katika mkoa wa Arusha Septemba 12,2018 ukitokea mkoani Mara.
Utapokelewa Olduvai Gorge kata ya Ngoile wilayani Ngorongoro.
Ukiwa katika mkoani wa Arusha utakimbizwa katika halmashauri zote 7 za mkoa.
Mwenge utaanzia kukimbizwa katika wilaya ya Ngorongoro,Karatu,Monduli, Longido,Arumeru na kumalizia Jiji la Arusha.
Mwenge ukiwa katika mkoa wa Arusha utakimbizwa umbali wa kilometa 1,114.9.
Utakagua,kuzindua,kufungua na kuweka jiwe la msingi miradi ipatayo 46 yenye thamani ya kiasi cha shilingi za tz 36,182,058,694.35
Ambapo mchango wa serikali Kuu ni Tsh 7,416,735,688.35, mchango wa wahisani mbalimbali ni Tsh 13,247,332,956, kutoka halmashauri michango ni Tsh 479,529,350 na michango ya wananchi ni Tsh 15,038,460,700.
Mwenge utaweka jiwe la msingi miradi 9,4 itafunguliwa,22 itazinduliwa na 11 itakaguliwa katika halmashuri zote.
Mwenge utamalizia kukimbizwa katika wilaya ya Arusha na kukabidhiwa mkoani Manyara Septemba 19,2018 katika wilaya ya Babati.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.