Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mtanda mapema leo hii katika kijiji cha Robanda Wilaya ya Serengeti.
Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Arusha umekimbizwa umbali wa Kilomita 1,168.47 na Miradi 62 yenye thamani ya sh. 47,290,543,421.83 imezinduliwa, kutembelewa, kufunguliwa na kuwekewa jiwe la msigi.
Michango iliyotumika katika miradi mbalimbali ya Mwenge wa Uhuru 2023 ni; sh.31,184,729,891.22 kutoka Serikali kuu, sh.1,657,992,282.09 halmashauri, sh.3,297,238,870.52 wahisani na sh. 11,150,582,378.00 wananchi.
Katika Miradi hiyo, 16 imewekewa mawe ya Msingi yenye thamani ya sh. 26,941,819,117.51.Miradi 14 imezinduliwa yenye thamani ya sh.11,206,373,826.32,miradi 8 imefunguliwa kwa thamani ya sh. 694,994,000.00 na miradi 24 imetembelewa na kukaguliwa kwa thamani ya sh. 8,457,506,478.83.
Mwenge wa Uhuru 2023,ulipokelewa kutoka Mkoa wa Kilimanjaro mnamo Juni 27,2023 na ukakimbizwa katika Halmashauri za Wilaya 7 za Mkoa wa Arusha na Julai 4,2023 umekabidhiwa kwa Mkoa wa Mara.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.