Mwenge wa Uhuru umepitia jumla ya miradi 8 katika halmshauri ya Meru nakuridhishwa na miradi hiyo.
Akizungumza katika hitimisho la ziara hiyo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bwana Abdalla Kaim amesema, miradi yote ipo vizuri katika halmshauri hiyo.
Mwenge wa Uhuru umepitia jumla ya miradi 8 ikiwemo ya Mazingira, afya, Miundombinu, shule na mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi iliyogharimu zaidi cha sh.bilion 8.7 na kati yake miradi 5 iliwekewa jiwe la msingi na miradi 3 ilitembelea.
Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Arusha zimekimbizwa katika halmashauri ya Meru na zitaendelea katika halmashauri ya Jiji la Arusha mnamo Juni 30,2023.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.