Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, vijana, ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Paschal Katambi (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda na kuzungumza Ofisini kwake Mjini Arusha mapemq leo Aprili 20, 2024.
Mhe. Katambi yupo mkoani Arusha kwaajili ya uzinduzi wa michezo ya Mei Mosi, kueleka kwenye Sikuku ya Wafanyakazi inayotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mhe. Katambi amempongeza Mkuu wa mkoa na wasaidizi wake kwa maandalizi mazuri kueleka siku ya wafanyakazi Kitaifa ambapo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye anayetarajiwa kuwa mgeni wa rasmi kwenye maadhimisho hayo.
Mh. Naibu Waziri Katambi pia amempongeza Mh. Paul Makonda kwa utumishi wake mzuri wakati akiwa Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi, akimsihi kuendelea kuwatumikia Wakazi wa Arusha bila ya kukatishwa tamaa na wasioitakia mema Tanzania.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda amemuahidi Mh. Naibu Waziri Katambi kuwa Ofisi yake itatoa ushirikiano wa kutosha kwa kamati zote za maandalizi ya kuelekea May Mosi ili kufanikisha sherehe hizo kwa namna ilivyopangwa.
Mara baada ya mazungumzo yao, Mh Mkuu wa Mkoa na Naibu Waziri Katambi walipata nafasi pia ya kuzungumza na Kamati mbalimbali za Maandalizi ya sherehe za siku ya wafanyakazi.
Mheshimiwa Naibu Waziri Katambi aliambatana na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya na Muwakilishi wa Kamishna wa Ajira,Ofisi ya Waziri Mkuu na Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Bwana Missaile Albano Mussa.
20April
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.