Waziri wa Mifugo na Uvuvi mheshimiwa Luhanga Mpina, ameiagiza bodi ya maziwa kwa kushirikiana na baraza la kilimo Tanzania kuandaa maonyesho ya kimataifa ya wiki ya maziwa badala kila mwaka kuadhimisha yakitaifa tu.
Ameyasema hayo alipokuwa akufungua maonyesho ya 21 ya wiki ya maziwa kitaifa, yaliyofanyika katika viwanja vya Themi Njiro jijini Arusha.
Amewataka kuendelea kusimamia sheria na kanuna za maziwa zinazotumika katika kila nchi, kwani soko la maziwa linapanuka kwa kasi sana.
Aidha, amesisitiza kuwa serikali inaendelea kuhakikisha inabadilisha sheria na kanuni ambazo zinaonekana hazina tija katika sekta hiyo, hii itasaidia sana katika uboreshaji wa soko la maziwa ndani na nje ya nchi.
Amewahasa wafugaji waendelee kutumia ufugaji wa kisasa kwani utaongeza uzalishaji wa maziwa kwa wingi nakutoa fursa zaidi za masoko kwa nchi za nje.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Arusha ameipongeza sana bodi ya maziwa kwa kufanikisha madhimisho hayo ya wiki ya maziwa na amewataka wazalishaji wazingatie zaidi sheria na kanuni za ndani na nje ya nchi ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima.
Magreti Kihumbuli mwakilishi kutoka bodi ya maziwa Kenya, ameishukuru bodi ya maziwa Tanzania kwa kuwapa mwaliko wakushiriki maonyesho hayo.
Amesema anatagemea kujifunza mambo mengi katika maonyesho hayo na hata pia waonyeshaji wa Tanzania watajifunza mengi kutoka kwao na hii itasaidia kuongeza uhusiano bora kati ya nchi hizi.
Luge Kawaga ni mwakilishi kutoka mamlaka ya endelezaji wa maziwa nchini Uganda, amesema maonyesho hayo yatasaidia kubadilisha elimu baina ya nchi hizo tatu.
Maonyesho ya wiki ya maziwa kitaifa yanafanyika mkoani Arusha kwa siku 3 ambapo makapuni takribani 40 yakiwemo ya kigeni yameweza kushiriki maonyesho hayo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.