Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameondoka Mkoani Arusha kupitia uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuelekea Jijini Dar Es salaam na kusindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christiana Makonda na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu, jioni ya leo Agosti 28,2024
Mhe. Rais amekuwa mkoani Arusha kufungua Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, Kikao kinachofanyika kwa siku tatu kwenye Kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.