Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega amewataka watanzania kupenda kutumia vitu vya kwao ili kukuza soko na kuvipa thamani.
Ameyasema hayo alipokuwa akifunga maonesho ya sherehe za nanenane kanda ya Kaskazini kwa mwaka 2020, jijini Arusha.
“Watanzania tumekuwa na kasumba ya kuthamini vitu vinavyotoka nje na kudharau vya hapa nchini, hii imesababisha bidhaa za ndani kukosa soko na thamani kwa ndani ya nchi na hata nje”.
Kanda ya Kaskazini inatakiwa kuwa ya mfano kwa kutumia bidhaa zinazozalishwa na gereza la Karanga kwani vitu vyake vina ubora na vinadumu.
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa ya kanda ya kaskazini Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti amesema maonesho ya kanda ya kaskazini yataendelea kuboreshwa zaidi ili kuhakikisha elimu inayotolewa ifike hadi ngazi za vijijini.
Maonesho ya sherehe za wakulima,wavuvi na wafugaji hali maarufu kama nanenane 2020 yalibeba kauli mbiu isemayo “ Kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi chagua viongozi bora 2020”.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.