Jumla ya washiriki 56 wa Mafunzo ya Mfumo Mpya wa Manunuzi ya Umma kwa njia ya Kielekroniki (NeST) Mkoa wa Arusha wamehitimu Mafunzo ya siku tano kwa Mafanikio.
Akifunga Mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi Usimamizi,Ufuatiliaji na Ukaguzi CPA.Ramadhani Madeleka amesema lengo kuu la Mafunzo hayo likukuwa ni kuwajengea uwezo Maafisa hao toka Halmashauri saba za Mkoa wa Arusha ili kuulewa namna ya kuutumia mfumo huo mpya wa manunuzi ya Umma ujulikanao kama NeST ili wakifika katika maeneo yao ya kazi wakawafundishe Maafisa wengine waliosalia namna ya kuutumia mfumo huu.
"PPRA walitoa Mafunzo kama haya kwa Maafisa toka Sekretariati za Mikoa yote Tanzania Jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwelewa wa kuutumia mfumo huu na kisha kuja kuwafundisha mafunzo haya ninyi Maafisa toka ngazi za Halmashauri,hivyo sisi kama Mkoa tunatarajia mtakwenda kuwafundisha mafunzo hayo Maafisa waliobaki katika Halmashauri zetu ili nao waweze kuutumia mfumo huu".
Sambamba na hilo,CPA.Madeleka amezitaka Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa ifikapo tarehe 15/09/2023 kila Halmashauri iwe imewasilisha taarifa yake ya kuelezea ukamilikaji wa mafunzo ya NeST kwa Maafisa waliosalia ngazi za Halmashauri na namna walivyoanza kuutumia Mfumo huu kwani ifikapo tarehe 30/09/2023 mfumo zamani hautatumika tena.
Aidha,amewataka Wakurugenzi wote wa Halmashauri kusimamia mfumo huu mpya wa manunuzi kwa kuhakikisha hakuna manunuzi yanayofanyika nje ya mfumo wa NeST kwani kuendelea kufanya manunuzi nje ya mfumo huu ni kosa kisheria na kuwa Halmashauri inatakayobainika kufanya hivyo itachukuliwa hatua za kisheria.
Mafunzo hayo ya siku tano kwa Mkoa wa Arusha yalianza tarehe 21/08/2023 na kufanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuhitumishwa tarehe 25/08/2023.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.