Shirika lisilo la kiserikali World Vision Tanzania limekabidhi miradi miwili ya Maji na Shule yenye thamani ya Milioni 820 kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha baada ya kumaliza ujenzi wake.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Kijiji cha Shambarai Burka kata ya Mbuguni kwenye mradi wa Kilimo cha umwagiliaji na mradi wa shule ya Kerikenyi kata ya Shambarai Wilayani Arumeru.
Akipokea miradi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Kimanta amesema juhudi zilizooneshwa na shirika la World Vision ni mfano wa kuigwa kwani linaisadia Serikali katika kuleta maendeleo mbalimbali kwa wananchi.
Aidha, Kimanta ameaidi wananchi wa Tafara ya Mbuguni kutatua changamoto zao ikiwemo miundombinu ya Barabara na umeme kwa kuhakikisha itafika katika eneo hilo.
Pia, amewataka wananchi hao kuanza ujenzi wa Zahati mapema na wadau watajitokeza kuwaunga mkono kama World Vision walivyowaunga Mkono kwenye ujenzi wa shule.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.