Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule ya Sekondari Embaseri Wilayani Arumeru inayojengea kwa fedha za TASAF.
Amesema mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inasaidia sana katika kutoa huduma kwa wananchi.
" Nimerishishwa na kasi ya ujenzi wa miradi ya TASAF niwaombe muendelee na spidi hii".
Nae, mratibu wa TASAF Mkoa wa Arusha bwana Richard Nkini amesema miradi yote ya TASAF kwa Mkoa wa Arusha ipo katika hatua za upauwaji na kupiga plasta.
Amesema kila halmashauri imepata fedha za TASAF takribani Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa, Matundu ya Vyoo, Ofisi za mwalimu, Majengo ya huduma ya Mama na Mtoto.
Dkt. Kihamia amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya TASAF katika Halmashauri zote za Mkoa kwa lengo la kujionea hali ya ujenzi wa miradi hiyo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.