Misa ya mazishi ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Marehemu Richard Kwitega, inaendelea katika kanisa la Katoliki la Mtakatifu Benedicto, Parokia ya Ngoma, wilaya ya Sengerema.
Misa hiyo takatifu inaongozwa na Askofu wa Jimbo la Geita, Muhashamu Askofu Flavian Kasala na kuhudhuria na maelfu ya waombolezaji na wakiongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, mheshimiwa David Silinde.
Aidha baada ya kukamilika kwa misa hii, waombelezaji wataelekea eneo la makaburi kwa ajili ya mazishi.
Marehemu Richard Kwitega, alikutwa na mauti akiwa safarini kuelekea mkoa wa Dodoma kikazi, kutokana na ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Mdori, wilaya ya Babati mkaoni Manyara.
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.