Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa nchini inayotegemewa katika suala zima la mzunguko wa fedha za kigeni, fedha ambazo zinatokana na shughuli za Utalii pamoja na biashara ya nchi jirani ya Kenya kupitia Mpaka wa Namanga.
Hayo yamebainishwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, wakati wa mazungmzo mafupi yaliyofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kilichowakutanisha Bodi ya Wakurugenzi wa BoT na Menejiment ya mkoa wa Arusha.
Gavana Tutuba amesema kuwa, kutokana na onhezeko la watalii mkoani Arusha, mkoa huo umekuwa ni sehemu inayotegemewa katika upatikanaji wa fedha za kigeni kutokana na wageni hao, kutumia fedha hizo kwa matumizi yao wawapo mkoani Arusha.
Amesema kuwa, BoT imeendelea kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa huduma za ubadilsihaji wa fedha nchini, huku mkoa wa Arusha ikiwa ni sehemu pekee ya kipaumbele kutoakana na mahitaji yanayotokana na idadi kubwa ya watalii wanaoingia na kutoka kila siku.
Aidha, Tutuba amempongeza Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani kupitia Filamu ya 'Royal Tour', ambayo matunda yake yameanza kuonekana wazi hususani kwa wakazi wa mkoa wa Arusha.
"Tunatambua Arusha, imekuwa ni kitovu cha Utalii, ikiwemo utalii wa mikutano ya kimataifa na kitaifa, mikutano ambayo licha ya kuongeza mzunguko wa fedha za kigeni, inasaidia kusaidia kurecover kwa uchumi lakini zaidi ni kichecheo cha ukuzaji wa uchumi wa taifa " Amesema Tutuba.
Hata hivyo, serikali imelegeza mashari ya mitaji na kugikia milioni 5 kwa wazawa na kuwataka wakazi wa Arusha kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwekeza mitaji kwenye biashara na kwa wenye hoteli za kuanzia nyota tatu kufungua maduka ya kubadilishia fedha ndani ya hoteli zao kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Hata hivyo Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, licha ya kumkaribisha Arusha Gavana Tutuba na Bodi nzima ya wakurugenzi wa BoT, amemuhakikishia hali ya usalama na utulivu wa mkoa wa Arusha, unaovutia wageni wengu kuendelea kuwepo Arusha.
Ameipongeza BoT kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kusimamia uchumi wa Taifa kupitia usimamizi imara wa fedha, unaosaidia mkoa wa Arusha licha ya kuwa na wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi, hakujawahi kutokea changamoto ya ukosekanaji wa fedha za kubadilisha.
Amebainisha kuwa, kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watalii nchini na kufanya shughuli nyingi za kitalii kufanyika mkoani Arusha, wananchi wa mko huo, wameendelea kunufaika na matunda ya filamu ya 'Royal Tour' ambayo imeongeza pato la mtu mmoja mmoja, familia, mkoa na Taifa pia.
Awali Gavana Tutuba yuko mkoani Arusha kwa shughuli za kikazi akiambatana na Bodi ya Wakurugenzi wa BoT ambao wanategemea kupatiwa mafunzo ya uendeshaji wa Bodi hiyo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.