Mkoa wa Arusha unatarajia kuwa mwenyeki wa Mkutano wa kawaida wa 22 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotajiwa kufanyika tarehe 22, Julai,2022 katika ofisi za Jumuiya huo.
Katika Mkutano huo nchi ya Jamhuri wa watu wa Kongo (DRC) itashikiri katika Mkutano huo ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki tokea ijiunge na Umoja huo.
Marais 7 wanatarajiwa kushiriki mkutano huo wakiongozwa na mwenyewe wao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ambae anatarajiwa kuwasili Mkoani Arusha hapo kesho tarehe 20 Julai,2022.
Aidha, wakuu hao wa nchi wanachama watazindua Barabara ya Afrika Mashariki ( By Pass) siku hiyo ya Tarehe 22 Julai,2022.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.