Na Prisca Libaga Arusha
Mkutano wa 77 wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, unatajiwa kufanyika mkoani Arusha kuanzia tarehe 20 Oktoba hadi tarehe 9 Novemba 2023, katika Kituo cha mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) Jijini Arusha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Rais na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Kamishna Remy Lungu akiongozana na Makamishna wengine na watendaji, amethibitisha kufanyika mkutano huo huku zaidi ya wajumbe 700 kutoka nchi za Afrika na Nchi wanachama wa Umoja wa nchi za Afrika wanatajiwa kushiriki mkutano huo Jijini Arusha.
Kamishna Lungu amesema mkutano huo utajadili masuala mbalimbali yanayohusu haki za binadamu na watu katika nchi za Afrika kwani bado changamoto nyingi za ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi hizo kwenye maeneo mbalimbali.
"Tumekuja kujadiliana juu ya haki za binadamu na tutoke na maazimio ambayo yatawezesha kila nchi kutekeleza ,siwezi sema sana nchi fulani inafanya vema kuliko nyinginezo katika masuala ya haki za binadamu kwakua kila nchi inamatatizo yake"
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu na Watu, Abiola Idowu Ojo alisema tume ya Afrika imewekwa idadi na utaratibu wa kukuza na kulinda haki kama ilivyoagizwa kufanya chini ya mkataba wa nchi za Afrika ikiwa ni pamoja na kuandaa vikao mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kusikiliza aina mbalimbali kuhusu haki za binadamu na maudhui.
"Tangu kuundwa kwa Tume hii imekuwa na mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya haki za Binadamu na Watu na imetoa mchango kwa kuimarisha usimamizi wa haki za watoto, wanawake na umiliki wa ardhi, haki zinazongatiwa na sasa lazima tuanishe changamoto zinazotukanili" Amesema Abiola Ojo
#ArushaFursaLukikuki
#KaziInaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.