Na Elinipa Lupembe.
Mwananchi wa kata ya Mateves halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, Mzee Samwel Sangeti, akiwasilisha kero yake kwa mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, akikilalamikia kijiji cha
Ngorbob kumdhulumu eneo lake na kulazimishwa na serikali ya kijiji kutoa shilingi milioni 30 alizolipwa fidia na Shirika la Umeme Tanzania -TANESCO, kuchangi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule mwaka 2020, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la soko la Kisongo Juni 04, 2024.
Kufuatia malalamiko hayo, Mhe. Makonda ameagiza kusimamishwa kazi Afisa Mtendaji wa Kata ya Mateves, Muyai Kivuyo kupisha ucbunguzi na kuvitaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa malalamiko hayo ili haki ya kila mmoja iweze kupatikana.
Mkutano huo umefanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, aliposimama kuwasalimia wananchi wa kata hiyo, wakati wa ziara yake mkoani Arusha Juni 02, 2024 na kumtaka Mhe. Makonda kurudi kwenye kata hiyo rasmi, ili kusikiliza na kushughulikia kero za wananchi hao wa kata ya Mateves.
#ArushaNaUtalii
#kaziinaendelea ✍
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.