Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa Marco Ng'umbi ameunda tume ya uchunguzi ili kujua nini chanzo kilichopelekea moto ulioteketeza na kuharibu bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Enduiment,
Ajali hiyo ya moto imetokea shuleni hapo Enduiment usiku wa Tarehe 26/8/2024, ambapo wananchi wa eneo hilo la Enduiment wakishirikiana na vijiji vya jirani walishirikiana kwa bidii ili kuzima moto huo bila mafanikio .
Bweni hilo la wasichana Enduiment linabeba zaidi ya wanafunzi 145,ambapo wakati wa moto huo unatokea wanafunzi walikuwa madarasani wakijiandaa na mitihani inayoendelea shuleni hapo
Aidha mkuu wa shule ya Sekondari Enduiment Mwalimu Hassan Hassan amezungumza na viongozi pamoja na wananchi waliofika mahali hapo na kueleza kuwa ,chanzo cha moto huo bado hakijulikani.Na yeye kama Mkuu alipokea taarifa ya uwepo wa moto huo kwa mwanafunzi aliekuwa anaumwa na amepumzika katika moja ya vyumba kwenye bweni hilo
Mwalimu Hassan ameendelea kusema baada ya kusikia taarifa hiyo walichukua hatua ya kupiga kelele na kelele zilizozaa matunda kwani wanafunzi wananchi wa maemeo ya karibu walifika kwa haraka na kuanza kufanya jitihada ya kuuzima moto huo kwa kutumia michanga na maji .
Sambamba na jitihada hizo zote ila bado hazikuzaa matunda kwani moto ulikuwa mkubwa na upepo ulikuwa mkali kiasi cha kushindwa kuokoa mali zilizopo kwenye bweni hilo zikiwemo vitanda ,magondoro na masanduku ya wanafunzi hao wa jinsia ya kike.
"Kwakweli vitu vingi vimeteketea mali zote za wanafunzi zimeharibika tumeokoa magodoro yasiyozidi hamsini tu"Alisema Mwalimu Hassan
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa Ng'umbi amewaomba wanafunzi, Walimu, wazazi pamoja na wananchi kuwa na subira na utulivu wakati Serikali inafanya uchunguzi juu ya moto huo na kutafuta namna ya kurejesha hali nzuri ya mazingira ya kuwawezesha wanafunzi hao kuendelea na shughuli zao za kawaida.
Ajai za moto zimekuwa tishio kwenye maeneo mengi,wananchi wanapaswa kuwa na uelewa juu ya namna ya kukabiliana na majanga ambayo yamekuwa tishio kwa binadamu na mali zao.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.