Wananchi wa kata ya Maloni wameishukuru Serikali kwa kuwajengea barabara yenye urefu wa Km 14.6, inayounganisha kata hiyo na barabara kubwa ya lami ya kutoka Waso - Sale, barabara ambayo licha ya kurahisisha usafiri imesaidia kufungua uchumi wa eneo hilo.
Wananchi hao wametoa shukurani zao, kwa wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, walipotembelea na kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi katani hapo, ikiwa ni zaiara yao ya kawaida ya kufuatilia utekezaji wa Ilani ya CCM.
wamesema kuwa, wananchi wa eneo hilo ni wanajishughulisha na kilimo na ugugaji, wakiwa ni wafanyabiashara wa mazao ya chakula na mifugo, hivyo uwepo wa barabara hiyo, licha ya kuwaondolea kero ya usafiri imewafungulia fursa za kiuchumi kwa kuwa sasa magari yaneweza kuingia na kubeba mazao hayo kupeleka sokoni.
Wamekiri kuwa, kwa miaka mingi waliteseka sana na kulazimika kutumia punda na pikiki kusafirisha mazao yao kwenda sokoni, jambo ambalo liliwagharimu fadha nyingi pamoja na muda, wa kusafiri kutoa eneo moja kwenda jingine
"Tunaishukuru Serikali ya Mama Samia, imetujali sana, ametuondolea kero kubwa kwenye kata yetu, tunasafirisha mazao, mifugo yetu kwa magari sasa, tunasafirisha wagonjwa kwa wepesi lakini hata watoto sasa wanakwenda shuleni kwa amani hasa ukizingatia eneo hili ni mbali na mji" Wamesema wananchi hao.
Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Loy Thomas Ole Sabaya, ameridhishwa na Utekelezaji wa Ilani ya chama katika kata hiyo na kuthibitisha kuwa Serikali ya CCM ina lengo la kutatua kero za wananchi nchini hususani wanainchi waishio vijijini kama ilivyo kwa wananchi wa Maloni.
Aidha, amewataka kuwa watulivu na kuendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita na viongozi wote wakiongozwa na Jemadari Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kujikita zaidi katika kufanya kazi za kujiingizia kipato ili kuinua uchumi wa Taifa lao la Tanzania.
"Niwaopongeze kwa kufanya kazi zenu za kilimo na ufugaji, niwasihii endeleeni kumuunga mkono Rais wenu Mama Samia na Serikali yake, amboyo inasisitiza kufanya kazi, mnajionea kazi kubwa iliyofanywa na serikali yenu, hivyo msimuangushe mama yatu mpendwa Samia" Amesisitiza Mwenyekiti Sabaya.
Awali, Kufuatia mkakati wa Serikali wa kuboresha miundombinu ya barabara vijiji, kupitia wafadhili wa KFW na TANAPA, imejenga Bararabara ya kiwango cha changarawe na kokoto yenye urefu Km 14, ya Mairowa - Njoroi kwa gharama ya shilingi milioni 884.6
Garama hizo zimejumuisha ujenzi wanmadaraja 4, structure 26 , drift 24 pamoja na eneo lililojengwa kwa kutumia kokoto, mradi unaowanufaisha wananchi 5,524 wa kata ya Maloni na wageni wanaoingia na kutoka katani hapo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.