• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

MSD NA WADAU WA AFYA WATAKIWA KUJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO YA UTOAJI NA UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA...

Posted on: November 29th, 2023

Na Elinipa Lupembe.


Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Wadau wa Afya wanaohudumiwa na MSD, wametakiwa kushirikiana kutoa mawazo ili kuwa na  mkakati wa pamoja, unakwenda kutatua changamoto za utaoaji na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, kutoka MSD, ili ziwafikie walengwa kwa wakati.


Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K. Mongella, wakati akifungua Kikao Kazi, kilichowakutanisha watalamu wa MSD na Wadau wanaohudumiwa na MSD, Kanda ya Kilimanjaro, kinachofanyika kwenye Hoteli ya Masaai Land mkoani Arusha.


Mhe. Mongella amesema kuwa, licha ya changamoto zinazoikabili Bohari hiyo ya Dawa, ameweka wazi kuwa, yapo mabadiliko makubwa ya utendaji wa Bohari hiyo, unaendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma ya dawa na vifaa tiba, kwenye vituo vya Afya vya mkoa wa Arusha.


Amesema kuwa kuna tofauti kubwa, ya uwepo wa dawa na vifaa tiba kwenye zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na hospitali za rufaa, jambo linalothibitisha utendaji kazi imara wa Serikali ya awamu ya sita, Wizara ya Afya na MSD, tofauti na vipindi vilivyotangulia hapo awali.


Hata hivyo Mhe. Mongella, amewataka wadau na watalamu hao, kupitia kikao kazi hicho kuja na suluhisho la kudumu la changamoto zilizosalia, katika kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana kwa wakati na kuwahudumia wagonjwa, huku wakitambua kuwa, Afya ni nguzo kubwa ya maendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.


"Serikali ya Mama Samia, imefanya kazi kubwa sana katika sekta ya Afya, na inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na MSD kwa sasa, tofauti na tulikotoka,  kikao kazi hiki kitoke na mipango ya utatuzi wa changamoto na sio kuziorodhesha, kazi kubwa mliyonayo ni kutoka na mbinu za ufumbuzi zijikita kwenye suluhisho la changamoto, ili kufikia malengo ya serikali" Amesema Mhe. Mongella.


Licha ya kupongeza kazi kubwa na nzuri inayofanywa na MSD, amewataka watalamu hao kutambua kuwa, malalamiko yanayoelekezwa kwenye sekta ya Afya, yanabainisha wazi, unyeti wa huduma wanayoitoa, kwamba inagusa moja kwa moja mahitaji ya jamii kwa mtu moja moja hivyo ni vema kuwa na mkakati thabiti wa kuondoa malalamiko hayo.


Aidha, Mhe. Mongella, amewataka  MSD,  kuimarisha mifumo ya TEHAMA katika utoaji wa Dawa na Vifaa tiba ili kuimarisha mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya nchini  pamoja na kufanya tathmin na kuhakikisha wanafanya kazi kwa pamoja ili kila upande uweze kutimiza wajibu wa kumhudumia mwananchi.

Awali Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa, 


Kikao kazi hicho cha mwaka, kinawakutanisha MSD na Wadau wanaohudumiwa na MSD wa mikoa ya kanda ya Kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.


#ArushaFursaLukuki

Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.