Mshauri wa Rais na Mwenyekiti wa Kamati ya Jukwaa la Kizazi chenye usawa Mh. Angellah Jasmine Kairuki (MB) amewasili mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha David Lyamonge kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha leo Agosti 19, 2024.
Mhe. Kairuki licha ya kusaini kitabu cha wageni amefanya mazungumzo mafupi na Kaimu katibu Tawala huyo na kueleza lengo la ziara yake mkoani Arusha.
Katika ziara hiyo, Mhe. Kairuki ameambatana na wajumbe wa Kamati hiyo, kutembelea halmashauri za mkoa wa Arusha lengo likiwa na kujionea jitihada za halmashauri katika uwezeshaji wa wanawake na wasichana
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.