Wakazi wa Mto wa Mbu Wilayani Monduli wametakiwa kuwa wakarimu kwa wageni hasa watalii kwasababu eneo hilo ndio kitovu cha utalii.
Yamesemwa hayo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mto wa Mbu.
Sekta ya Utalii ni muhimu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yetu, hivyo ni muhimu kuwakirimi watalii wanaokuja ili waweze kutamani kurudi tena.
Dkt. Mpango amesisitiza kuwa Monduli hasa eneo la Mto wa Mbu ndio lango la utalii kwa Mkoa hivyo lazima waweke mazingira mazuri yakuvutia watalii.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.