Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 Godfrey Eliakimu Mnzava amekagua na kuweka Jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa barabra ya Olasiti kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 3.96 inayojengwa na kampuni ya Jiaxi Geo Engineering (group) Julai 22, 2024.
Mnzava ameweka wazi kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara ili kila mtu aweze kufanya shughuli zake za kiuchumi bila kipingamizi.
Amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Arusha kuzikutanisha Tasisi za maji AUWSA, umeme TANESCO, TARURA pamoja na Halmashauri kukaa pamoja barabra hiyo ikamilike kwa wakati na huduma zote zipatikane na wananchi wanufaike kama yalivyo malengo ya Serikali
Mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 4.9, ni miongoni mwa barabara zinazotekelezwa kupitia mradi wa uendelezaji na uboreshaji Miji na Majiji kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (TACTIC) lengo likiwa ni kusogeza huduma za miundombinu ya barabara kwenye makazi ya watu ili kurahisisha usafiri na kupunguza gharama za usafiri.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.