*MAKABIDHIANO*
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella akimkabidhi funguo za gari, aina ya Toyota Land Cruser - Ambulance, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Mhe. Saimon Laizer , wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya magari ya Afya, iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha leo tarehe 05.12.2023.
Akikabidhi Magari hayo, Mkuu huyo wa mkoa, amewasihi viongozi wa ngazi zote, kusimamia utunzaji na matumizi sahihi ya vitendea kazi hivyo, ili viweze kufanya kazi iliyokusudiwa na Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi na sio kinyume na hivyo, huku akiwasisitiza kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassani ya kufikisha huduma karibu na wananchi.
"Viongozi mnalo jukumu kubwa la kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki, wafuatilieni watendaji wa Serikali katika maeneo yenu, hakikisheni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi unawanufaisha wananchi, wananchi wanahitaji suluhu ya changamoto zao kupitia sisi, wahakikishieni utendaji wa serikali yao kwa vitendo" Ameweka wazi Mhe. MoMongell
#ArushaFursaLukuki
#Tunatekeleza
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.