Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzani (TIC), Dkt. Binilith S. Mahenge, amefika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha nakupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. John, V.K Mongella leo tarehe 18 Januari, 2024.
Akiwa ofisini hapo, Dkt. Mahenge amesaini kitabu cha wageni na kufanya mazungumzo mafupi na mkuu wa mkoa huyo pamoja na kueleza malengo ya kufika mkoani Arusha.
Dkt. Mahenge yuko mkoani Arusha kwa lengo la kufanya Kampeni ya Kitaifa ya kuhamasisha Uwekezaji kwa Watanzania wazawa, kampeni ambayo iliyoazinduliwa rasmi na Waziri Mkuu mwezi Septemba 2023.
Amesema kuwa, kampeni hiyo, ina malengo makuu mawili ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusu dhana ya uwekezaji, kuwahamasisha watanzania kushiriki katika na kuondoa fikra na mtazamo potofu kwa kwamba wawekezaji ni wageni kutoka nje ya nchi.
Hata hivyo, Mhe. Mongella amemkumkaribisha Mkoani Arusha na kumuahidi kutoa ushirikiano wa kuhakikisha Kampeni hiyo inafikia malengo ya serikali ili watanzania wazawa waweze kutumia furasa hiyi kuwekeza ndani ya nchi yao.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.