Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko amewasili Mkoani Arusha jioni ya leo na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha na Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye kwenye Kiwanja cha Ndege wa Kimataifa cha Kilimanjaro Aprili 13, 2024.
Naibu Waziri Mkuu yuko Mkoani Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa Kituo cha Kurushia Matangazo ya Redio (TBC Taifa na Bongo FM), kwenye uwanja wa Kassim Majaliwa uliopo Wasso-Loliondo wilayani Ngorongoro, Aprili 15, 2024.
Aidha, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dotto Mashaka Biteko (Mb) atazindua Kituo hicho kwa niaba ya vituo vingine vya Makete, Kyela, Uvinza na Mbinga.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.