Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Jumanne Oktoba 8, 2024 amewasili Jijini Arusha na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ambapo Kesho Jumatano Oktoba 09, 2024 Naibu Waziri Mkuu anatarajiwa kufungua Mkutano wa mwaka wa wataalamu wa Mionzi barani Afrika, Mkutano unaofanyika kwa siku tatu kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Jijini Arusha AICC.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.