Na Prisça Libaga Arusha
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko amesema Maafisa mipango ndio moyo wa Taasisi yoyote hivyo kuwataka wanafanye Kazi zao kwa Lengo la kupanga mipango thabiti kwa maendeleo ya jamii na Taifa.
Dkt Biteko ameyasema hayo wakati akimuwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye ufunguzi wa Kongamano la wanamipango linalofanyika kwa siku Tano Mkoani Arusha na kuwataka maafisa hao kutumia Taaluma zao kuleta maendeleo.
Amewataka kuwa na mipango ya Muda mrefu inayotekelezeka ili kuhakikisha nchi inapiga hatua kwenye sekta mbalimbali wanazosimamia na hivyo wananchi nao wanapata maendeleo.
"Maafisa mipango ndio moyo wa Taasisi na jukumu lao ni Kubwa hasa kwenye kupanga na kuhakikisha mipango hiyo inatekelezeka kwa wakati ulipo na hata miaka ya baadae" amesema Biteko.
Kongamano hilo la siku nne linafanyika wa mara ya kwanza tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipounda Wizara ya Mipango na Uwekezaji
Pamoja na mambo mengine wataalamu hao watajadili namna ya kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo.
Awali Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof.Kitila Mkumbo amewataka Maafisa Mipango kuanza Maandalizi ya mpango mpya wa Taifa wa maendeleo baada ya Mpango wa Sasa kufikia tamati mwaka 2025.
Prof Mkumbo ametoa Kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo la Wanamipango 2023 na kusema kuwa uandaaji wa Mpango mpya wa maendeleo wa Taifa utafanywa na Maafisa hao.
"Tunaandaa mpango mpya wa Taifa wa maendeleo ambao unaanzia mwaka 2026 wahusika wakuu wa uandaaji wa Mpango huo ni nyie ambao Leo mmekuwa hapa na hivyo kila Moja wenu ajiandae kwa Kazi hiyo".alisema Prof Mkumbo
Kwa Upande wake Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba amesema kwamba sekta ya Mipango huwezi kuitenganisha na sekta ya fedha hivyo kila Moja wetu anao wajibu wa kutumia sekta ya mipango kwa maendeleo ya Taifa letu hivyo wajibu wetu kila Moja kujua na kutumia mipango ya maendeleo kwa matumizi sahihi ya Rasilimali.
Nae Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema kwamba kada ya mipango ni muhimu sana ikaendana na mipango ya maendeleo yenye muelekeo Moja ndio maana wizara hiyo inao mfuko wa maendeleo ya barabara unaokusanya karibia bilioni 600 kwa maendeleo ya barabara zetu.
Maafisa mipango kutoka halmashauri Taasisi za umma wizara na idara za serikali wanakutana kwa siku nne Mkoani Arusha kwa Lengo la kujadili namna Bora ya kupanga maendeleo katika taasisi zao.
Kauli mbiu ya Kongamono hilo ni "Fikra za pamoja na utekelezaji ulioratibiwa kwa ustawi jumuishi"
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.