Na Elinipa Lupembe
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amekikabidhi hati milki 30 za ardhi kwa wananchi walionunua viwanja kupitia Mradi wa Safari City, unaotekelezwa na Shirila la Nyumba la Taifa (NHC), Jijini Arusha, Oktoba 24 Oktoba 2024
Katika eneo hilo, jumla ya hati 240 zimeshagawiwa kwa wanunuzi wa viwanja katika mradi huo, ambapo Naibu Waziri huyo amekabidhi hati milki 30 kati ya 81 zilizoandaliwa.
Hata hivyo Mhe. Pinda ameliagiza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kujenga nyumba zenye hadhi kulingana na uhitaji hususani katika maeneo ya mijini na kusahurinkuwa na mpango mbadala kuzibomoa nyumba za zamani za katikati na kujenga za kisasa.
‘’Vijumba vingine vilivyopo kati kati ya mji kwa kweli ni kama vile vya urithi, havina sura ya Tanzania ya sasa, muende mkaweze upya ili tupate thamani inayofanana na uhalisia, ukiweka hata ukumbi utapata wapangaji wengi, ukijenga mahoteli watu watakuja kupanga na kuendesha shughuli zao’’. Amesema Mhe. Pinda
Naye Meneja wa NHC mkoa wa Arusha Bw. Benit Masika amesema, hadi sasa SHirika limeweza kuuza jumla ya viwanja 1,026, kati ya hivyo viwanja 350 wateja wake wamemaliza malipo kwa 100%.
"Kwenye mradi wa Safari City, HNC imetenga viwanja 1,601 kwa ajili ya kuviukuza kwa lengo la kutoa fursa ya uendelezaji kwa wananchi wazawa na wadau na viwanja 313 shirika limehifadhi kwa ajili ya uendelezaji wa baadaye’’. Amesema Masika
Ameongeza kuwa, mradi huo tayari umefikiwa na huduma wezeshi kwa wateja kama vile maji, umene pamoja na miundombinu ya barabara aliyoieleza kuwa, imekuwa ikiendelezwa na serikali ili kuwawezesha walionunua maeneo kuendeleza maeneo yao na wanunuzi wa viwanja wamefurahi na kuishukuru Serikali kwa kuwakabidhiwa hati milki za ardhi katika eneo ambalo limepangiliwa vizuri.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.