Naibu Waziri wa Maliasili Mhe. Dustan Kitandula Agosti 4, 2024 amefungua Mkutano wa 109 wa Waesperanto uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa AICC na kubudhuriwa na mataifa zaidi ya 63 ikiwa Tanzania ni nchi Mwanachama.
Mkutano huo ni miongoni mwa mikutano inayoendelea kufanywa na Waesperanto katika kukuza lugha ya Kiesperanto duniani. Akiongea katika ufunguzi wa Mkutano Mhe. Naibu Waziri ameeleza kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania na Arusha kwa ujumla utasaidia kuendelea kufungua fursa ya kiutalii nchini ikiwa ni ajenda ya Taifa katika kukuza Utalii wa Mikutano.
Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huo mkubwa wa Waesperanto kufanyika nchini Tanzania na kupokelewa vizuri. Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amewakaribisha wageni wote kutoka mataifa mbalimbali na kueleza ajenda ya Mkoa ni kuendelea kukuza Fursa za Kiutalii ikiwa ni pamoja na utalii wa Mikutano kama uliofanyika na Waesperanto.
Aidha katika ufunguzi huo Serikali ya China imetoa zawadi kwa Serikali ya Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na kueleza zawadi hiyo inathaminika sana kwa nchi ya China na inahifadhiwa katika Maeneo ya Makumbusho.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.