Na Elinipa Lupembe
Naibu Waziri wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihanzile (MB) amefika kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha na kupokelewa na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Albano Musa.
Naibu Waziri huyo, amesema kuwa yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kawaida ya kikazi ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya Kiwanja cha Ndege Arusha eneo la Kisongo Jijini Arusha.
Mhe. Kihanzile ameweka wazi kuwa, lengo la Serikali kukarabati na kuongeza miundombinu ya kiwanja hicho ni kuwa na miundombinu rafiki yenye uwezo wa kuwahudumia wasafiri sambamba na kupokea idadi kubwa ya wasafiri, kutokana na uhitaji mkubwa wa wasafiri wanaofika mkoani Arusha ikiwemo watalii wa ndani na wale wa kimataifa wanafanya safari za ndani ya nchi.
Akizungumza na Naibu Waziri huyo, Katibu Tawala mkoa wa Arusha amemkaribisha na kumshukuru kwa kufika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kumuhakikishia hali ya amani na usalama wa mkoa huo kwa sasa hukua akiahidi ushirikiano kipindi chote atakachokuwa kwenye mkoa huo.
Hata hivyo Katibu Tawala huyo, amethibitisha umuhimu wa Kiwanja cha ndege cha Arusha kwa wakazi wa mkoa huo pamoja na wageni wa ndani na nje ya nchi, hivyo hakusita kuipongeza na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kupanua miundombinu ya uwanja huo, ambao licha ya kutoa huduma za usafiri lakini unachangia ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Arusha na wananchi wake.
"Kwa sasa Kiwanja cha Arusha kinahudumia wasafiri wengi kwa siku, kikiwa na watu wanaofanya safari za ndani ya nchi na ndani ya mkoa wa Arusha, kuna ndege ndogo za watalii wanaokwenda kutembelea mbuga za wanyama na wapo watalii wanotoka mbugani kuelekea Zanzibar, kwa idadi hiyo kubwa ya wasafiri uwanja huo unatakiwa kutoa huduma zake kwa saa 24 za siku". Amebainisha Afisa Tawala huyo
Ikumbukwe kuwa ukarabati wa miundombinu ya kiwanja cha ndege ni utekelzaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi Ibara ya 68 2020 -2025 inayoelekeza serikali kuimarisha miundombinu ya utalii ikiwemo kujenga na kukarabati barabara zilizopo ndani ya maeneo ya vivutio vya utalii, mmadaraja
njia za miguu, viwanja vya ndege.
#ArushaFursaLukuki
#KaziInaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.