Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amemtaka Mkuu mpya wa Wilaya ya Karatu Mhe. Dadi Horace Kolimba kwenda kuhakikisha mji wa Karatu unapangiliwa vizuri.
Maelekezo hayo ameyatoa baada ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan mnamo Disemba 4,2021.
"Mji wa Karatu unakuwa kwa kasi sana na usipopangiliwa mapema huko baadae utakuwa mji wa msongomano na usivutie watalii Tena".
Amewaaidi kuwapa ushirikiano wa kutosha ili wote kwa pamoja waweze kutimiza matarajio ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Dadi Kolimba amesema amepelekwa Karatu ili akasukume maendeleo hivyo ameomba ushirikiano uliotukuka kwa viongozi wa Serikali, Chama na wananchi wote.
Nae, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Said Mtanda ameaidi kutoa ushirikiano uliotukuka kwa watu wote na hata kuwaheshimu.
Sherehe za uwapisho huo ulifanyika kwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Karatu na Mkuu wa Wilaya ya Arusha alipewa nafasi ya kuzungumza machache na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama na Dini walihudhuria sherehe hizo wakiwemo wakuu wa Wilaya wenyeji wa Mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.