Katibu Tawala mkoa wa Arusha Dkt.Athuman Kihamia leo ameitisha kikao kazi cha uboreshaji utoaji wa huduma za afya kati ya RHMT, wakurugenzi wa halmashauri zote saba za mkoa wa Arusha pamoja na waganga wakuu wa halmashauri hizo.
Dkt.Kihamia amesema malengo makuu ya kikao hicho ni kuimarisha utoaji huduma za afya kwa ngazi zote za halmashauri, kuimarisha usimamizi kwa kusaidia mawasiliano na mahusiano mazuri kutoka ngazi za juu hadi chini na pia kuweka mikakati ya kutatua changamoto zilizopo katika halmashauri hizo.
Aidha pia Dkt.Kihamia amewaambia wakurugenzi na watendaji wote wanakaribishwa ofisini kwake ikiwa kuna changamato naye atazitatua kwa haraka.
Mganga mkuu wa mkoa Dkt Silvia Mamkwe amewasilisha taarifa nzima ya afya kwa mkoa wa Arusha katika utoaji wa huduma na ujenzi wa vituo vipya.
Pamoja na hayo Dkt.Mamkwe amewaomba watendaji wote wa halmashauri kushirikiana kikamilifu kutekeleza miradi yote.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.