Leo Ijumaa Julai 12, 2024 imefanyika Parade kubwa Jijini Arusha yenye kuhusisha Madereva wa pikipiki kutoka Mkoani Arusha wanaotarajiwa kushiriki kwenye Samia Motocross Championship inayofanyika kwenye Viwanja vya Laki laki Kisongo Jumapili Ya Julai 14, 2024.
Parade hiyo ni maalum kuelekea kwenye michuano hiyo ambayo mshindi wa kwanza anatarajiwa kuchukua Milioni 10 za Kitanzania, mshindi wa pili Milioni 7 na Mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi Milioni tano.
Hakuna kiingilio kwenye Mashindano hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ametumia mashindano hayo kuwaalika wananchi wa Mkoa wa Arusha kutumia vyema fursa ya wingi wa wapenzi wa mbio za pikipiki wanaotarajiwa kushuhudia michuano hiyo ya Samia Motocross Championship.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.