Ujumbe wa Program ya imarisha uchumi wa Mama Samia inayohusisha makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye mahitaji maalum, ikiongozwa na Mshauri wa Rais Masuala ya wanawake, vijana na makundi maalum Sophia Mjema na kukukutana na makundi ya wanawake, kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Agosti 20, 2024.
Ujumbe huo, umewakutanisha makundi hayo kwa lengo la kupeana fursa mbalimbali za kibiashara na kuboresha uchumi wao kupitia program maalum ya mikopo isiyokuwa na riba.
Akizungumza na wanawake hao, Sophia ameyataka makundi hayo, kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo Mkoani humo, huku akiwatambulisha programu mpya ya kitaifa ya Imarisha Uchumi na Mama Samia.
Ameongeza kuwa, timu hiyo inazunguka Tanzania nzima kutambua majukwa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi kuanzia ngazi ya kata, wilaya na mkoa ili kujione namna mamlaka za Serikali zinawawezesha kiuchumi kama yalivyo malengo ya Jukwaa.
"Kutakuwa na utaratibu wa kujiorodhesha kwenye kanzu data ya kuwatambua mahali vikundi vilipo, jinsi ya kuvifikia pamoja na kutambua shughuli zinazofanywa na vikundi na majukwaa hayo" Amesema Sophia
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wanawake kiuchumi Beng'i Issa amesema kuwa lengo la programu hiyo ni kubaini changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na wajasiriamali hao, ili kuwa na mkakati wa kuleta suluhisho la changamoto hizo na kuwainua kiuchumi.
Aidha, amewataka wanawake wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa ya utalii ambao ndio uchumi wa mkoa huo, kwa kuwahimiza kujiingiza kwenye soko la utalii wa mikutano ambao umekuwa kwa kasi Arusha.
Hata hivyo wajasiriamali hao wamelalamikia changamoto ya mitaji na soko na kuiomba Serikali kuwasaidi kutatua changamoto hizo ili kuingia kwenye ushindani na wafanyabiashara wakubwa.
Paulina Sayot Mjasiriamali kutoka wilaya ya Karatu ameomba kuwepo na utaratibu wa watalii kupita kwenye biashara zao ili nao waweze kufanya biashara na watalii kama ilivyo kwa wafanyabiashara wakubwa.
Naye Shamimu Msangi amesema kuwa, licha ya kendelea kupambana na changamoto za masoko lakini pia ukosefu wa mtaji wa kutosha na maeneo maalum ya kufanyia biashara bado ni changamoto hivyo ujio wa programu hiyo utawakamboa wajasiriamali wengi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.