Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kila mmoja kujipima kwanamna gani anadhibiti rushwa ili kuleta maendeleo ya mtu mmoja moja au taifa kwa ujumla.
Amewataka nchi zote wanachama wakatekeleze maadhimio yaliyopitishwa na Mkutano huo ili kudhibiti kabisa maswala ya rushwa kwani vinazolotesha maendeleo ya nchi zetu.
Afrika inatakiwa kuonesha Dunia kuwa bara hili sikichaka chakuficha fedha za rushwa au wala rushwa bali ni bara ambalo si salama kwa wala rushwa.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 48 kati ya 50 zilizosaini Mkataba wa kutekeleza Mkataba wa umoja wa Afrika wa kupinga rushwa mnamo mwaka 2005.
Jukumu la kutokomeza rushwa nilakila Mtanzania hivyo kila mtu ajitazame mwenyewe na kujifanyia tathimini.
Amesema, nchi ya Tanzania imeweza kuokoa kiasi cha sh. bilioni 39 fedha ambazo zingepotea kupitia mazingira mbalimbali ya rushwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menenjimenti ya Utumishi wa Umma George Simbachawene amesema, maadhimisho hayo niya 20 katika utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Afrika wa kuzuia na kupambana na rushwa ambayo yanafanyika kila mwaka.
Maadhimisho hayo yameambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo matembezi yakupinga rushwa, Kongamano na vipindi vya kuelimisha katika vyombo mbalimbali vya habari.
Tanzania itaendelea kusimamia taasisi zote zinazoshughulika na mapambano dhidi ya rushwa kwa pande zote mbili bara na visiwani ili kuhakikisha rushwa inamalizwa.
Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU Salim Hamduni, amesema kupitia maadhimisho hayo wameweza kutoa elimu juu ya rushwa na kubadilishana uzoezi baina ya nchi na nchi na hivyo kupelekea kila nchi kujifunza zaidi kutoka nchi nyingine.
Pia, maadhimisho hayo yamewasaidia kuongeza zaidi ushirikiano baina ya nchi hizo na kuweka nguvu zaidi juu ya kupambana na rushwa.
Maazimishi hayo ya mapambano dhidi ya rushwa kwa bara la Afrika yamehudhuriwa na nchi takribani 24 kutoka bara la Afrika.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.