Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema serikali itawalipa fidia wananchi wote waliovamia na kuweka makazi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA).
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa USA river wilayani Arumeru alipokuwa njiani kuelekea uwanja wa KIA.
Dkt.Samia amesisitiza zaidi kuwa ingawa waliovamia eneo hilo ni wananchi wenyewe lakini kutokana na kuwa wameshaweka makazi yao ya kudumu katika eneo hilo serikali ikaona ni vyema iwalipe.
Amesema Serikali imeshatenga fedha takribani bilioni 11 kwa ajili ya kuwalipa wananchi wa hao.
Eneo lenye mgogoro limejuisha vijiji 7 kutoka kata ya Kia kuna vijiji Chemka,Rundugai,Sanya Stesheni, Tindiga na Mtakuja vilevile kutoka kata ya Arumeru vijiji ni Malula, Samaria na Majengo.
Katika vijiji hivyo vile vitakavyoonekana vipo ndani ya eneo la uwanja ndio watakaolipwa fidia.
Mgogoro huo wa mpaka umedumu kwa zaidi ya miaka 20 na eneo hilo lina ukubwa wa Kilomita za Mraba 110.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.